Hecko mwalimu wetu, baraka twakumiminia

Published by M Johnson on

Shangwe na vigelegele, Furaha mpwitompwito
Wangeni wetu karibuni, Mstarehe bila wasiwasi
Twasherehekeha mwalimu wetu, kweli amutupa ushindi,
Hecko mwalimu wetu, Baraka twakumiminia.

Shukrani twatoa kwa mola, Mwalimu wetu aliyetupa
kwako wewe twajifunia, milele ta kukumbuka
Ijapokuwa twakuaga, Mioyoni mwetu hutoki,
Hecko mwalimu wetu, Baraka twakumiminia.

Kwa wingi hukosi maarifa, kwa sifa wafahamika,
Ulitusomeshaaa, Ulituelekeza,
Ukaturekebisha, Ukitufaamisha,
Naaaaaaa
Ukatuhamasisha!….. ukituchekesha,
Hecko mwalimu wetu, Baraka twakumiminia.

Waona , kuliko wa rika letu, maarifa kweli unayo
Chumvi nyingi ulokula wewe, kamwe sisahahu na jamii,
Uwaelekeze vijana, uwarekebishe wasichana,
Ukiwafahamisha kinamama, nakuwahamasisha kinababa,
Hecko mwalimu wetu, Baraka twakumiminia.

Kaditamati twafika, hayaishi haya mawazo
Shukrani twatoa kwa mola, kwa kutupamwalimu wetu,
Milele humioyoni mwetu, kwa mema ulotutendea,
Hecko mwalimu wetu, Baraka twakumiminia.

Categories: Ushairi